Breaking News

REAL LOVE 💘....SEHEMU 3 ( LOVE STORY Tamu na ya Kusisimua)

ILIPOISHIA.....
Nikamkuta kakaa kitako akisapotiwa na mto akinitazama kwa ukali sana pindi nilipokuwa ninaingia......
ENDELEA..........
"Mambo da Leyl@th... "
Nilijikuta naanza kumchangamkia mgonjwa ambaye muda wote alikuwa akinitazama kwa umakini nadhani alikua anatafakar aliponiona lakin hakupata jibu,
"Safi tuu "alijibu kwa uvivu hivyo hivyo lakin skujali,
"Nimekuletea uji, sijui utaweza kunywa? "Nikauliza huku nikiwa natoa vifaa nolivyokuja navyo Kama chupa, kikombe na kijiko,
"Asante "alijibu kwa unyonge sana,.. nikamimina uji kwenye kikombe kisha nikaanza kumlisha huku nampigisha story za uongo na ukweli ilimrad acheke cheke kidogo,kusema ukweli nina uzoefu wa kumuuguza mtu kwani mama yangu huwa namuuguza mwenyewe tokea nipo mdogo,
"Vp uji mzito!?? "
"Hapana Ndo mzur, Asante sana,"
"Aah Ucjal,"niliendlea kumlisha huku nikimchekesha na vibonzo tofaut tofaut,
"Leyl@th "
"Abee"
"Swadaktaa, jina lako unalkumbuka eee "
"Yaah but vitu ving sielew elewi, "
"Usijali utarudisha kumbukumbu zako tu Sawa, "
"Sawa! "Alijibu kwa unyonge sana
"Mim naitwa Sancho Mlatino, A.K.A ,Albino mwenye gundu, "
"Hahahah afu Wew "
"Nin jaman "
"Kuna albino mweusi "
"Cndo Mim sasa viungo vyangu havina dili "
"Kweli viungo vyako siyo dili, so Wew mim unanijua? "
Swali lake lilinifanya nicte kutoa jibu,
"Hahahah we si Leyl@th! "
"Ndio mim Mbona sikukumbuki, "
"Usijali utakumbuka tuu, "tukawa tunapiga story mbili tatu kuhusiana na Maisha yake lakin alionekana hakumbuki vitu ving Kwan alisahau hadi wazaz wake walipo, hata namba ya simu ya Mtu hata mmoja,tukiwa katika maongez yaliyo mfurahisha zaid mgonjwa, daktar aliingia,
"Habar za jion jaman, naona mgonjwa kafurahi sana, "
"C huyu apa nani.. sancho ananichekesha "
"Hahahah vizur, nimekuja na hivi vdonge vya kurudisha kumbukumbu jitahid umeze sasa hivi kisha upumzike,
"Doctor akinywa hivyo Ndo kumbukumbu yake itarudi eee "niliuliza kwa shauku sana,
"Yaah kumbukumbu yake itakua inarudi kidogo kidogo lakin jitahid kuwa nae karibu na umuulze maswali tofaut tofaut kuhusiana na yeye, naa... ningependa tumuache apumzike kidogo"
"Sawa doctor, "
"Yaah Wew nenda kamuandalie chakula cha usiku then mletee "
"Sawa nmekuelewa,Leyl@th,"
"Abee "
"Utakula ugali,? "
"Mmmm chips bhna "
"Okee Sawa si chips kavu ee "
"Vyovyote tuu "
"Haya baadae eee "
"Sawa "
Nikatoka nikiwa najifikiria jinsi ya kuzipata hizo chips anazozitaka yeye maana mfukoni sent 5 sina na sijui nitaipata vipi jion Kama ile, nikiwa napita zangu chochoro za kurud nyumbani, nikashtukia nikiitwa,
"Oyaa sancho Mlatino vp "
"Daaah vip Suma "
"Shwar tuuu naona upo hai hai sijui unawahi wapi "
"Daaah mwanang we acha tuu yan apa kwanza nashkuru kwa kukuona ndugu yangu, "
"Umeanza vizinga damu yangu "
"Siyo vizinga Ismail ujue Wew Ndo Kama ndugu yangu kaka matatizo yangu yote unayaelewa suma "
"Sawa sancho mwanang Sema leo mim sijauza kabisa maji mwanang si unaona madumu yamejaa Haya mpaka now, enhe kuna nini? "
"Mama hajala tokea mchana ndugu yangu "
"Daaah bas Siyo kes mi nina jero mwanang, hapa nilipo nmechoka naenda kulaza mkokoteni, "
"Shukrani kaka itasaidia tuu Usijali "
"Pamoja Mlatino mwanang "
"Poa Poa kaka "...niliondoka haraka haraka huku nikianza kuipigia bajeti ile mia tano, nikapata wazo la kupitia gengeni kwa Mully,nikapita chochoro zangu nikafika fasta,
"Oya Mully inakuaje "
"Kama kawa mwanang albino mwenye gundu "
"Ivoo yani, Sema nin ujue, nina shida "
"Nilijua tuu mwanang kwa shida nimekuzoea, Haya jielezee "
"Bi maza hajala mwanang, Kwahyo Nataka viazi mbatata vile, nyanya nyanya masalo, kitunguu na ndimu kaka "
"Duuh unashiling ngap? "
"Nifanyie kibingwa tuu shilingi mia tatu "
"Daaah sancho una makuz mwanang nakupa viaz vitatu "
"Daaah Mully vitatu havitoshi mwanang mwenyewe nataka nidundie hapohapo "
"Asa mia tatu mwanang,hata ivyo nakupa vukubwa vikubwa, "
"Basi nakupa jero fasta Nifanyie vingivingi hata vikiwa vidogo vidogo "
"Hahahah kumbe hela unayo "
"Amna mwanang we unanichinja tuu "
"Usiwaze mwanang, nimekuwekea hadi vya kesho "
Kutokana na kulalamika kwangu Mully alinipa viaz ving vilivyotosha kupika chips na hata viaz vya kula mama, nikarud nyumbani haraka haraka nikiwa na vitu vyangu, moja kwa moja nikaelekea chumbani kwa mama,nilijikuta nimeganda huku nikiwa nimeduwaa na mwili ukianza kutoa majasho mengi baada ya kumkuta mama yangu kipenz anatokwa na damu nying na akiwa amelala kana kwamba hajitambui...... itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA KWA DABEST TZ 

Post By: Dabest Tz

No comments