REAL LOVE 💘......SEHEMU 23
REAL LOVE
ILIPOISHIA......
Aliongea mama akituacha mim na Leyl@th tuliokuwa tukitazamana......
ENDELEA......
"Leyl@th..... "nikajkuta naita,
"Abee, "
"Sijui nikushukuruje kwa msaada wako ndugu yangu,... yani..... hata sijui nisemeje Dadaangu, "
"Sancho mim ndo napaswa kukushukuru kwa kuokoa maisha yangu Sancho una... "
Alisita kidogo,
"Nin Leyl@th!?? "
"Unanafasi kubwa ndani ya moyo wangu, kila mara nilishi nikiwaza jinsi gan nitakupata, sancho wew ndiye uliyeuteka moyo wangu kila nilipoumwa na hata baada ya kupona ulibaki kuwa kumbukumbu isiyopotea akilini mwangu,, naku..... yani nakushukuru sana Sancho,"
"Nashkuru kwa kunikumbuka na hili kubwa kuliko wangu... vip hali yako kiujumla, "
"Sancho mi nimepona kabisa ,si unaona nakumbuka kila kitu, "
"Kweli umepona manaake ulivyojirudisha kama Beyonce yule wa Jay nani sjui, "
"
"Vituko gan wakati mim nakuja nikakuona nikawa najiuliza huyu miss Tanzania kwenye haka ka jumba kadhahabu kafata nn "
"
"Na hilo lubega sijui kakufunga mama maanayake... "
"Mi susemi "
"Usiposema mmbeya "
"Haa! Kwan leyla mmbeya? "
"Leyla mim
"Siyo wew, yule aliyeimba langu rohoni,
"Mmm mi siskilizagi taarabu "
"Basi ndo maana huwajui wambea, "
Tukajikuta tunakatisha maingoz baada ya Mama kuingia na chakula,
"Sancho mwanangu hebu lete maji ya kunawa! "
"Acha tu, nifate Sancho "alidakia Leyl@th,
"Mwaka huu boss mim "
"Boss wa nn mwanangu makopo au "
"Hahahah
"Asa mamaako ndo analeta hela, umeambiwa, "
Tukaendelea kujibizana mpaka Leyl@th amiporudi na maji kwenye bakuli moja ya plastic,
Tukanawa kisha tukaanza kula kimya kimya kama ilivyo desturi mpaka tukamaliza, Leyl@th aliinuka kutoa vyombo nami ikabibidi niinuke kuchukua maji ya kunywa jikoni ambapo kuna kagiza Fulani kutokana na makuti mengi yaliyoezekwa na udogo wa kachumba hako, nikiwa nachota maji kwenye ndoo kubwa ya maji safi nikashtukia kiuno changu kimeshkwa na kuanza kupapaswa tarabitu, nikageuka na kumkuta Leyl@th aliyekua ananiangalia kwa macho malegevu mno, kabla sijasema kitu nilishtukia lips zangu zimevamiwa na kuanza kunyonywa kwa ufundi sana mpaka nikajikuta nagairisha zoez nilokua nikilifanya, na kuanza kujibu mashambulizi ya kupeana lita za mate,mala Leyl@th alionekana akishtuka sana huku akiwa kama anasikilizia kitu,
"Vipi? "
"Simu yangu inaita,wait kdogo "alitoka haraka kuelekea chumbani kwa mama kulipokuwepo vitu vyake akaichukua huku nami nikirudi na maji ya kunywa, alisikika akiongea lugha ngeni maskioni mwangu hata kwa mama pia, ila Mwisho akasema Sawa,
"Jamani baba kaniita niwahi, ningeomba niwaache, "aliongea huku akiondoa lile lubega na kubaki na kimini kimoja matata, hakika Leyl@th ni chotara haswa kwani ana kasura kakichaga, anashepu ya kihaya,mguu wa kinyakyusa, nyonga ya kidigo, mgongo wake uliokua wazi ulionyesha wazi ulikua ni wakimanga na hipsi pana za kindengeleko, hakika nywele zake na rangi yake ndo ilikua ya kiarabu, mchanganyiko wa vitu huvi vilimfanya aonekane mzur kama siyo wa sayari hii,
"Mama bye, sancho Naenda, "
"Ngoja nikutoe hata nje"
Nikaweka maji yale kisha nikaanza kufatana naye japo alitembea kwa mwendo wa haraka, nami sikuwa nyuma mpaka tulipofika alipopaki gari yake, akapanda,akawasha,... "take this phone honey! "aliongea kizungu huku akinikabidhi Simu ya Nokia zile za kawaida,
"Nitakutafuta mim Sawa "
"Sawa Asante sana "
Akaondoka kwa speed kali sana, hakika alionekana kutigwa kama mtu aliyepata taarifa mbaya..... itaEndelEaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA WWW.DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments