REAL LOVE 💘......SEHEMU 22
REAL LOVE
ILIPOISHIA.......
Nilimchukua suma haihai tukawa tunaelekea nyumbani ambapo siyo mbali, kufika nyumbani nikashangaa na kujikuta nasimama baada ya kumkuta Leyl@th imesimama mlangoni kwetu anatokea ndani.......
ENDELEA........
Alitoa tabasam pana huku akituangalia sisi tuliokuwa tunakuja kasi,
"Eh! Sancho vipi leo waarabu mzee?!! "
Aluniuliza suma huku akimtazama Leyl@th ambaye kavalia khanga na kajifunga lubega kana Kwamba anaonekana alikua anashughuli anafanya,
"Leyl@th!!
"Yes Sancho
"Ni wewe? "
"Yaah mim "
"Mbona upo hivyo? "
"Nipoje "
"Umevalia khanga hiyo ya... "
"Hee kuvaa kanga ya mamaang jaman kosa? "
"Mamaako gani "
"Hee Vibaya kwan Sancho?! "
"Aaa.. amna Yaani nilitaka kujua umepajuaje hapa "
"Nikuulize wew umepajuaje hapa Sancho!? "
"Hapa mim si kwetu! "
"Na mim hapa kwetu, karbuni ndani "alifunga maongez Leyl@th aliyekua akinijibu kimzaha japo majibu ya mkato mkato, tukaingia ndani huku suma akionekana kuniminya minya akiwa haamini kama Mlatino nlkua naongea na toto la kiarabu,
Tulifika hadi kwa mama tuliyemkuta anafagia chumba chake na kumfanya Suma aliyeonekana kushangaa na kuduwaa kabisa,
"Mama
"Ismail mwanangu "
Alimkumbatia mama huku akiwa haamini,
"Mama unauongea,? "
"Ndio mwanangu Ismail "
"Daah mungu mkubwa sana "
"Amin mwanangu njooen ndani kidogo "
Tukaingia wote watatu Yaani mim mama na Ismail tukamuacha Leyl@th ambaye alikua anatuangalia kisha nikamuona anaelekea jikoni,....
"Wanangu mnajisikiaje kuniona hivi, "
"Daah amani sana bimkubwa "
"Furaha mama "
Tulijibu kila mtu na jibu lake,
"Kwanza nashkuru kwa kuwaona mpo pamoja bado, naomben mzdishe umoja wenu mpendane sana, kwan hata mim nafarijika kuwaona hivi, mim niliwamic tuu kuwasalimu Wanangu mnaweza kuendlea na shughuli zenu "
"Mama Yaani mi nina furaha sana leo, sema nina oda ya madumu ya maji wacha Nipeleke kisha nitarud "aliongea Ismail huku akisimama,
"Sawa mwanangu kazi kwanza mi kwakua nipo Ucjal sana "
"Sawa mama,.. Sancho ee mida mida kama vipi! "
"Poa mwanangu kama wew hakunaga si unajua, "
"Najua mwanangu kama ww hajatokeaga "
"Ebu tokeni na maneno yenu yakihuni msnichekeshe bure, "alidakia mama,
"Haya mama mi Naenda "
"Haaya "
Akatoka Suma na kuniacha na mama pekee,
"Vipi mwanangu huko mitaani lakini manaake siku nying kweli, "
"Huko fresh tu mamaang, vipi niambie huyu Leyl@th kapajuaje hapa "
"Mmm mwanangu una haraka wew, ...Haya ipo hivi, nilipoumwa siku ile doctor mmoja hiv mnene kias, "
"Hancy "nilidakia,
"Enhee huyohuyo alikuja nae ndipo wakanichukua wakanipeleka dukani kununua mavaz ndo nimeletwa nao hapa,
"Anhaaa Yaani nasemea... "kabla sijaongea aliingia doctor Hancy pamoja na Leyl@th wakiongozana,
"Ahaa bwana Sancho vip za tokea jana,"alinisalimu doctor Hancy kwa shangwe nying,.
"Salama tu doctor nashkuru sana kwa yote kaka maana nilikwama sana yani hata sijui mama yangu angepona ponaje,
"Hahahah Sancho Leyl@th ndiye mtu pekee wa kushukuriwa kwan yeye ndiye aliyetoa malipo yote ya operation tena express inayotumia advanced equipments zilizofanikisha zoez hilo japo tatizo halikuwa lile tulilokwambia mwanzoni,... tatizo lilikua dogo sana Yaani kuna sensory neuron ambayo huchukua taarfa na kupeleka kwenye ubongo kwaajili ya kurudisha taarfa ya kufanya tendo husika kama kutembea, kuongea, asa hiyo prosess ya neurons activity ilifail nadhani kutokana na mshtuko mkubwa alioupata tokana na msongo wa mawazo so cha msingi ni kumuinsist amalize dozi ili hilo eneo lipone kabisa then baada ya miez mitatu arudi kwaajili ya kutolewa nyuzi,"
Alielezea doctor Hancy kwa urefu zaid,
"Kwahyo tatizo ilikua ni kuitengeneza hyo nanii tuu "
"Yaah tena siyo kuitengeneza ni kuirudisha katika special system yake ili iendelee kufanya kazi yake kama unavyomuona "
"Daah shukrani sana,... nikamgeukia Leyl@th aliyekuwa ananitazama baada ya kuona namuangalia akainama chini,
"Basi mama mi ningeaga nilienda kufata dawa hizi ndo nimeleta, so ningeomba nirudi kwenye majukumu yangu tafadhali,
"Aaa Sawa kwaher "tulimuaga doctor kisha akatoka,
"Mama ngoja niwaandalie chakula "
Alijisemea Leyl@th huku akisimama,
"Heee mwanangu ebu kaa niandae mwenyewe leo nihakikishe kama nimepona kweli "
Aliinuka mama na kutuacha mim na Leyl@th tuliyokuwa tukinitazamana.......itaEndelEaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA WWW.DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments