REAL LOVE 💘......SEHEMU 24
REAL LOVE
ILIPOISHIA......
Aliondoka kwa speed kali hakika alionekana kutingwa Kama mtu aliyepata taaarifa ya mbaya..........
ENDELEA...........
Taratibu nikaanza kujikongoja kurud nyumbani moja kwa moja hadi chumbani kwangu nikajitupa kitandan huku furaha iliyojazana moyoni haikuwa na kifani, nikawa naichezea cm aliyonipa Leyl@th na kujarbu kubofya sehemu tofaut ili kujitoa ushamba, nilisikia nikiitwa na mama, nikatoka kuelekea chumbani kwa mama,
"Vip kumbe umerud? "
"Mda Mbona mama "
Nilijibu huku nikiendlea kuchezea cm,
"Hee una cm mwanangu "
"Hahahah mambo ya Leyl@th hayo mama "
"Anhaaa alafu mwanangu, kwan huyu mwarabu umemuotea wap maana..... "
"Daah mama huyu storia yake ndefu sana"
"Ndo uniambie hyo story na mim nijue, "
"Kuna siku nilkua zangu napita nikawa napiga story na muuza miwa Barbara ile ya kuelekea magomen, yeye akaja na gari yake pemben akapaki akaja kununua miwa huku kashka chupa ya maji, sasa ile anaondoka mim nikamuomba ile chupa ya maji akanipatia bila hiyana, asa alivyoondoka mi nikaendlea na misafara yang nafika hapo magomen kama unaelekea mwembe chai, nikakuta ajali, kuangalia vizur ndani ya gari moja ile ile aliyokuja nayo kwenye miwa,haraka haraka nikaenda nikamtoa nikamuwahisha hospital wakaanza kumtibu lakin alipoteza kumbukumbu kwa ujumla ikabidi mim ndo niwe ndugu yake maana hakuna ndugu yake mwenye taaarifa naye na hakumbuki hata namba zao.., bas mim ndo nikawa namplekea chakula mpaka akawa hajambo hajambo, simu ya kuruhusiwa namfata akawa amechukuliwa na ndugu zake
"Mmmh mwanangu una moyo wa huruma sana, sasa ikawaje mpaka mkaja kukutana tena, "
"Mama mi mwenyewe nimeshangaa kajuaje unaumwa wakati naskia alisafir wap Dubai cjui vile, ".
"Alikwambia nan? "
"Kuna doctor mmoja mnene mnene hivi aliyekuletea dawa ,
"Anhaaa huyo ndo alikujaga nae leo "
"Bas ndo hivyo ".. ..ilinibidi kumuelezea mama mkasa mzima juu yang na Leyl@th,
"Haya mwanangu kuwa nae makin usije ukamuudh mtoto wa watu, acha nipumzike maana huu mshono hapa na hiz dawa znanilevya naona "
"Haya mama "nikatoka kuelekea chumbani kwangu na kunitupa kitandan na kujikuta naingia kwenye dimbwi la mawazo juu ya Pendo "sijui kaibiwa Kweli ama alkua ananizuga"nilijiuliza mwenyewe bila kupata jibu sahihi, nikawa naendlea kuchezea cm huku nimelala, nikajkuta nimepitiwa na usingiz mnono na wenye uchovu sana,.. nilishtushwa na mlio wa cm uliotoa sauti ya wimbo wa msanii wa bongo fleva Nilipoangalia nilikuta namba iliyoandikwa wife material na picha ikatokea ya Leyl@th , nikapokea,
"HELLO...."
"EEE HALOOO "
"UPO WAP SANCHO,? "
"NIPO NYUMBANI HAPA"
"ANHAAA BASI FANYA HIVI, CHUKUA BAJAJ MWAMBIE AKULETE VATICAN CITY HAPA SINZA, "
"AAA SAWA BASI NGOJA NIJIANDAE FASTA FASTA"
"HAYA BAS USCHELEW "
"USIJALI MI MJESH "
"HAYA... "akakata cm, moja kwa moja nikaelekea nje kukinga maji kwa jirani ambapo ndipo nachotaga, nikarud haraka haraka hadi chooni nikawa naoga faster faster ilimrad kutoa jasho, nikamaliza nikarud ndani kutafuta nguo yenye muonekano kuliko Zote nikaipata suruali moja ya jeans ya kizamani ya mikasi mikas nikaichukua nikaivaa, nikachukua na shati nikalitinga bikachukua na raba zangu ambazo zlikuwa za marehemu baba,nikatoka kwa mwendo wa haraka kuelekea barabara ya tandale sinza, nikawa napita zangu chochoro nikasikia mtu akiniita japo hakutaja jina langu,
"Weee.....wewee... wew "
nilipogeuka nikamwona Honestry akitembea kwa haraka huku anachechemea kuniwahi,nikasimama,
"Mambo vip dadaang"
"Safi tu unaelekea wap?"
"Kuna sehemu naenda mara moja, "
"Kwan Unaharaka sana? "
"Yaah Vipi kwan "
"Nina mazungumzo na wew marefu kidogo sema nipe namba yako ukirud utaniambia,...taja namba "
"Daah mi namba yangu yenywe siijui "
"Lete cm yako "
Nikaitoa cm yangu na kumkabdhi cm yangu nikamuona anaandika namba zake kwenye cm yangu kisha akapiga kwake ilipoita akaisevu namba yangu kisha akanirudishia cm yangu,
"Isave namba yangu inaishia 81"
"Poa "nikajibu huku nikianza kuondoka nikiangalia jins ya kusevu nikashndwa nikaachana nayo, nikawahi BAJAJ iliyopita nakuismamisha,
"Oya inakuaje suka? "
"Kama kalanjunga boss wangu niambie "
"Nataka unipeleke SINZA vatikani siti "
"Anhaaa panda twende"
"Sh.Ngap maana hamkawii kusema laki Nyinyi, "
"Hahahah
Nikapanda tukaanza safar ambayo ilichukua dakika tano tukawa tumefika, niliposhuka tuu nilisikia cm yangu ikiita mklio ule niliousikia mwanzo nilipotoa kuangalia alikuwa Leyl@th namba yake inapiga ,nilishtushwa baada ya kupikea na kusikia sauti ya kiume,
"OYA UPO WAP WEW "
Nilijikuta nimeganda nisijue cha kujibu ........ItaEndelEaaaaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA WWW.DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments