Breaking News

REAL LOVE 💘....(+18)SEHEMU 8

REAL LOVE 💘....(+18)SEHEMU 8
ILIPOISHIA..........
Ikanibidi niende kufungua huku nikiwaza ni akina nani na wanataka nn usiku ule... nilishtuka baada ya kuona wanaume wawili waliojazia sana....
ENDELEA......
nikavuta pumzi kishujaa kisha nikatoka nje,
"Oya Mlatino tumekuchoka mwanang daily unatuzungusha mzigo wetu asa huu mguu cyo wa kisenge Kama huna chetu, tunaanzisha mbungi,"aliongea jamaa mmoja ambaye nakumbuka niliwadhulumu shilingi elfu kumi yao na nikawa nawazungusha, lakin leo nilishangaa kuwaona mlangoni kwangu nikiwa natafakari nani aliyewaelekeza kufika kwetu pale,
"Kwahyo ela yetu unatoa au "
Alinikuda jamaa mwengine ambaye ckumjua tokana na rangi yake kuwa nyeus sana,
"Daaah wakubwa ela yenu mnapata, "
"Toa ela sasa hivi "
"Msiwaze wanangu mbona Star mim leo mchana nimekutafuta maskani yako ili nikuungie Sema skukuzoom "
"Ulikuja wapi Wew mizinguo inakatika mwezi sasa ela yetu unatupiga chenga unajifanya messi, sasa leo Lete sound uone tunavyokuwashia mziki ukeshe nao na Dj Star Kama kawaida "
Ile mikwara ilinifanya nijiulize mwenyewe kimoyo moyo Kama ningekua ndo sina je cjui ingekuaje yani nadhani ningepata dozi mpaka niweke historia,
"Poa niachie niwachukulie fasta "
"Dakika mbili tuuu ukichelewa tunakutimbia umo umo, nikaingia ndan nikachukua noti moja ya elfu kumi kati ya zile tano alizonipa Rahma,
"Haya mzigo wenu huu apa wazee, "
"Unabahati leo Mbona tungeondoka na kibanda chenu hichi, "
Waliondoka huku wakiwa wanakikashfu kibanda chetu kisichokua na mvuto chenye bati upande mmoja upande mwingine kinaudongo, humo ndan giza jingi tokana na makuti yaliyoezekwa juu ya nyumba, kusema ukweli kibanda chetu kile hakina hadhi ya kuishi mjini Kwan kinaharibu Muonekano wa mji, taratibu nikajikongoja had ndan nikafunga mlango nikajitupa kitandani, tokana na msongo wa mawazo meng yaliyoshindwa kupishana na kusababisha ajali nying kichwani mwang mpaka nikachukuliwa na usingiz mzito mpaka asubuhi saa tatu na nusu, niliamka nikaenda kumjulia hali kipenz mama Yang aliyekuwa pia yu mzima wa afya, nikarudi kufagia fagia maeneo tofaut tofaut ya bandani kwetu kisha nikajiandaa kwa ajili ya kwenda kumchukua Leyl@th, hakika siku hyo kijumba chetu kilikua kidogo kina Muonekano Kama vile panakuja kutembelewa na rais,nikawasha moto kisha nikainjika sufuria ya maji ya chai, nikaenda kumchukulia mama vitumbua vya mama Rody ambavyo hua anavipenda sana ,nikarudi nikakuta chai inachemka nikaipua nikammiminia kwenye kikombe akaanza kunywa huku nampa story mbili tatu,
"Mama leo naenda kukuletea toto la kiarabu apa, mama alionickiliza kisha akatabasamu sana,
Nilipata faraja sana kumuona mama akiwa katika hali ya furaha japo haongei, nilimlisha kidogo kisha nikamuaga nikatoka kuelekea hospital, sikukawia sana Kwan nilipanda daladala ,nikashuka nikaelekea had hospital, nikapokelewa vzur na daktar yule anayemhudumia Leyl@th,
"Karibu sana ndugu yangu "
"Asante sana vp mgonjwa wang yupo tayari maana nmekuja kumchukua,
"Haa mbona alkwisha chukiliwa!!! ".....itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABEST4G.BLOGSPOT.COM

Post By: DabestTz

No comments