Breaking News

REAL LOVE 💘.....(+18)SEHEMU 10


REAL LOVE 💘.....(+18)SEHEMU 10
ILIPOISHIA......
"Vip ndugu yangu za masiku?!! "
"Aah salama tuu "
"Daaah Ebhana ndugu Yule dada wa wa kiarabu anakuulizia sana yan hapa kanipa kazi nikutafute ww kivyovyote........ "
ENDELEA.......
Nilishtushwa na taarifa ile ambayo ckuitegmea kwa wakati ule,
"Ameniulizia lini?!! "
"Wiki sasa imepita ndugu yangu, lakin alinambia nikikupata nikupe namba zake umtafute au nimjulishe Kama nimekupata, "
"Duuh mim sina cm kusema ukweli Kama utaweza kumjulisha cyo mbaya, "
"Basi Ngoja nimpigie now "
Nikabaki nangojea kwa shauku sana huku nikiwa nawaza meng juu ya Leyl@th...na doctor nae alionekana anabonyeza cm yake kisha anapiga, alijaribu mara kadhaa kufanya hvyo lakin pia haikua Sawa ,
"Vp tena?!! "
"Daaah hata hapatikani kwenye namba zake zote alizonipatia, "
"Tunafanyaje sasa?!! "
Akiwa anajaribu tena akakuta inapatikana,
"Uyoo inapatikana, eee hallo madam, vp haali, sasa ipo hivi yule mtu nmempata,..... Daaah sasa itakuaje?!!.... nimekutana nae njian tuu,... haya nitajitahidi."
Alionekana doctor kupata mshangao baada ya kuongea na cm hyo iliyosemekana ni Leyl@th....
"Vp anasemaje, "
"Anasema yupo Airport anaelekea Dubai, "
"Anarudi lini?!! "
"Baada ya wiki mbili "
"Vp hali yake? "
"Hali yake ni mzima kabisa kiujumla yani anakumbuka kila kitu yani kapona "
"Duuh sasa inakuaje, "
"Wew endlea na mishe mishe zako alafu baada ya hizo wiki mbili njoo hospital pale tutajua tunampataje, "
"Daaah haya bhna...."
Ama Kwel ng'ombe wa masikini hazai, niliondoka nikiwa nimenyong'onyea sana, nguvu ya kuokota makopo ilinipotea kabisa nikajawa na dimbwi la mawazo,nilwaza sana kwann anitafute na kwann ckupata taarifa hizo mapema tuu,
"Daaah mamae mi Kwel Albino mwenye gundu😔 "
Nilijkuta njisemea kimoyo moyo, nikaendlea na safar yangu kuelekea nyumbani ambapo nilimkuta kipenz mama yangu akiwa amelala, nilimuamsha lakin alionekana kuchoka sana nikamuacha nikaelekea gengeni kwa Mully,
"Oya mlatinoo!! "
"Inakuaje Mully damu yangu!? "
"Ivo ivo ktaani Mwanang upo vizur, "
"Nipo vzur na nn ndugu yangu Maisha yenywe daily hayabadliki "
"Maisha hayabadliki wapi wakati huonekani "
"Sionekani c natafuta makopo ckuhz adimu kchizi yan, "
"Hahahah haya bhna ulkua unataka nin? "
"Nipe bamia la mia mbili, nyanya moja tu na nyanya chungu za mia Mwanang "
Akanifungia akanikabidhi,
"Poa Poa Mlatino c tupo"
"Nasa Mwanang Pamoja sana "
Nikaanza safar ya kurud nyumbani ambapo syo mbali na hapo gengeni, nikarudi home nikapika haraka haraka ili mama akiamka akute chakula teyar, nikamaliza nikasonga ugali mlaini ambao mama hupendlea sana, nilpomaliza kuivisha nikaelekea chumbani kwa mama ambaye nilimkuta tayari keshaamka Kama dakika chache zilizopita,
"Vp mamaang unajickiajee, aliitka kuonyeshea yupo Sawa,
"Ngoja nilete chakula tule bas mamaang,... nikaandaa chakula kile maji ya kunywa na ya kunawa kisha nikaanza kumlisha mama Kama ilivyo kawaida yangu kusema ukweli mama yangu nilimzoesha hivyo yan lazma nimlishe tonge mbili tatu kisha yeye mwenyewe anaendelea, tukala pale tukamaliza nikawa nampigisha story japo hakushriki kunijibu chochote kwangu ilikua faraja sana kukaa naye tuuu na kuongea ongea nae ili kupoteza mawazo yangu ya kumkosa Leyl@th kwan matumaini ya kumpata yalianza kupotea taratibu, kutokana yeye alivyo mzur na maisha yake ni mazuri japo sikujua kwao papo Vip lakin picha halisi ya ufahar wa maisha yao ilinijia kichwani mwangu, nilikaa sana na mama siku hyo mpaka ikatimia saa moja usiku,
"Hivi mama usiku utakula tena nikuandalie? "
Alikataa kwa kutikisa kichwa, nikammbleza lakin alionekana kushba sana, nikamuacha, nikatoka nje ili kutembea tembea kidogo, nilizunguka nyuma ya mtaa kuelekea kwa kina Ismail ambaye nimimkuta akiosha mkokoteni wake wa kuuzia maji,
"Vip ndugu yangu "
"Ahaa nambie sancho Mlatino "
"Kama kawaida mbaba inshu vipi? "
"Umeadimika ndugu yangu "
"Amna kak mishe mishe tuu "
"Vp mama lakin "
"Ivyoo ivyo tuu,
Maongez yetu yalikatishwa na piki piki moja iliyokuja na kufunga break kali mbele yetu, ilibaki kidogo tumtukane kwa gadhabu lakin niligundua ni Yule dereva aliyenileta usiku ule natoka kwa Rahma,
"Sancho Mwanang unahitajika "aliongea kwa pupa bila hata ya kutusalimu kias alinifanya nianze kupata hofu....... itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments