Moto wa Messi, Suarez ni Balaa
Lionel Messi na Luis Suarez
BARCELONA ilikuwa na MSN ikiwa ni muunganiko wa wachezaji watatu wa
mbele, wakawa wakali katika mabao, lakini licha ya kuondoka kwa Neymar
kwenda Paris Saint- Germain, bado ‘majembe’ mawili yaliyosalia yamekuwa
hatari kwenye ufungaji mabao.Kuondoka kwa Neymar kukafanya wabaki MS yaani Lionel Messi na Luis Suarez, wawili hao kwa pamoja wamefunga mabao 42 katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.
Messi akiwa na mabao 22, Suarez ana 20 katika msimu huu, idadi hiyo ni kubwa kiasi kwamba wamezizidi timu 74 katika ligi kuu tano kubwa za Ulaya.
MS kwa jumla wamefunga mabao 53 katika michuano yote, Messi akiwa na mabao 30 wakati Suarez ana 23.


No comments