Diamond Kupiga Shoo Kombe la Dunia 2018
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz.
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz anatarajiwa kushiriki katika
wimbo maalumu wa Kombe la Dunia nchini Russia. Wimbo huo utakuwa
unawakilisha bara la Afrika.Wimbo huo umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.
Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka Machi16 mwaka huu.



No comments