REAL LOVE 💘.....SEHEMU 33
REAL LOVE
ILIPOISHIA.......
Nikamshangaa macho yakizidi kubadilika na kua mekundu sana ,Hakika mapigo yangu ya moyo yalikwenda kasi sana kama feni za ndege.......
ENDELEA........
Nikaanza kurud nyuma taratbu taratbu lkn nikajikuta naongeza kasi baada ya kusikia miungurumo ya simba kutoka kwa pupa huku nimeshika nguo zangu mkononi, nilistaajabu kukuta bonge moja la geti lenye kuta ndefu sana hakika niligundua ni mijengo ya waarabu au wahindi, nikaanza kuvaa haraka haraka huku nikitafakar pa kutokea, nikafungua geti mara ya kwanza ukakataa, nikaongezea nguvu zangu kulivuta mpaka likaachia nikatoka nikajikuta nipo eneo moja ambalo haliishwi na watu hata mmoja, moyo wa hofu ulikwishaanza kunijaa kwani sikujua hali ya leyl@th itakavyokua na mashetani yake, na mim nielekee wap kwani hata nilipokua naelekea sikujua nitarokea wap,kwa mbali sana nilimuona mtu akija na pikipiki, kadiri alivyokarbia kwangu nilipata kutambua kuwa alikua ni Nuuran, akafika kwangu mie ambaye nilikwishasimama,
"Vip Shemej dada hali yake
"Daah mbaya sana yan afu kanambia nikimbie mi hata sipajui yan nimechoka vibaya "
"Panda nikuwahishe Shemej "
Hakika sikujivunga na pozi zilikimbia, nikapanda haraka haraka kama mmasai wa kenya,
"Vipi leyl@th sasa humfati tena "
"Usijali nitamrudia "
Aliendesha kwa mwendo kasi kama tupo kwenye ndege, alitumia speed nyingi hadi nikawa sion vitu pembeni tokana na upepo unaonipiga usoni, nilishtukia nimerushwa huko tokana na mshindo wa gar ulioigonga pikipiki yetu na kuanguka, nilijitahidi kuinuka lakini sikuweza kabisa, nikaishiwa nguvu na kupoteza fahamu kabisa,.................
nilifumbua macho majira ya saa kumi jioni ambapo nilishtukia watu wakizozana lakini Syo kwa lugha ya kiswahil ,nikajiinua taratbu, nilishangaa sana kujikuta nipo kwenye ile nyumba niliyomkimbia leyl@th, nikazid kutazama kwa makini lakin hakukuwa na tofauti yoyote kwakweli, mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio baada ya kukumbuka kua nilipata ajali na Nuuran, nilijaribu kuinuka lakin sikuona tofauti yoyote katika mwili wangu,
"Ooh Shemej
"Vipi unajisikiaje Mpnz now "
"Salama tuu vipi kwan "
"Shwari tuu, karibu tena duniani
Kauli yake iliniachisha mdomo wazi kwan sikujua A wala Z,...... ItaEndelEaaaaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABES4G.BLOGSPOT.COM

No comments