Breaking News

REAL LOVE 💘.....SEHEMU 29


REAL LOVE 💘.....SEHEMU 29
ILIPOISHIA........
Nilipofika nilimuona alikaa na leyl@th ambaye aliniangalia kwa jicho kali sana na nilistaajabu kuona nawasalimu lakin yeye akatoa msunyo mkali..........
ENDELEA.......
"dadaaa 😒,ndo nn sasa! "
"Niache Nuh, "
"Mmmh bas sawa, Shemej Karbu ukae "
"Shemej, Shemej.. Shemej yako atakua huyo maskini mmalaya mmoja annanif.....alidakwa mdomo na Nuuran ambaye hakutaka aendelee kuongea maneno yake yote kwan yalionekana makali sana kias nami yaliniingia na kulifanya chozi langu kuanza kudondoka taratbu nikiwa siamin kama leyl@th angeweza niambia maneno yale ya dharau "
"Kosa langu mim lipi Jaman, nimewaudh wap, umasikini wangu ndo unifanye nitukanwe kias hiki, yaan hili ndo mloniitia 😪Nashkur sana Nash... 😭kuuruu "niliongea kwa uchungu sana huku nikiwa ninajutia hali yang ya umasiki moyo wangu ulihamia kwenye kumbu kumbu ya maisha yangu kiujumla ,nikajikuta nageuka naanza kuondoka huku machoz yakinitoka kama mtoto aliyechukuliwa pipi yake,
"Sancho.. Shemej "aliniita Nuuran lakin sikusimama nikawaacha wakilaumiana kiarabu lakin Nuuran ndo alisikika kana yeye ndo anamlaumu leyl@th ,moja kwa moja nikaelekea kituoni nikachukua gar za kuelekea kwetu nikapanda, kwakweli macho yalikua mekundu sana kwan kila nilipokumbuka kauli ya leyl@th nilijikuta naishiwa nguvu, nilijawa na msongo wa mawazo kichwani hadi nikashtukia nimepitishwa kituo, nikashtuka baada ya dada mmoja aliyekaa siti ya pembeni yangu kunishtua,
"We kaka! 😳,Mbona unalia? "
"Amna nipo sawa "
"Hee kweli dunia hadaa 👌😌"
"Kivip! 😒"
"Kumbe watu wapo wa aina nyingi eee "
"Aah mi ckuelewi! "
"Amna yani kuna watu ambao wakilia ndo wapo sawa na wakiwa hawalii ndo hawapo sawa eee "
"Amna kawaida, 😨nimepitishwa "
Nilijikuta naropoka baada ya kuona nimefika kinondoni karibia na mkwajuni,
"Refaa refaaa.... nilijikuta naropoka kama chizi mpaka nikawa nimesahau jina la muhusika,
"We nin mwanangu umechanganyikiwa nn "aliongea jamaa mmoja aliyeonekana ndiye konda kwan alishika chenj chenj nyingi,
"Daah samahani nilisahau konda mmenipitisha 😐"
"Tumekupitisha vipi sema we ulikua unashuka wap "
"Kona au garrage "
"Si umeona ulivyotingwa, Mbona hapo ndo tulikua tumesimama kuna folen pale kwenye ajali au naongopa Jaman "
"Kweliiiiii...... '''''''' "waliitikia abiria wengne,
"Bas Njoo ushuke hapa studio utafute gari za kurudia huku, nikasimama kisha nikawa najitahidi kupenya penya ili nishuka lakin cha kushangaza nikaona yule dada akinifata nyuma,nikashuka na kuvuka barabara haraka,
"Hey kakaa "
Aliniita yule dada niliyekua nimekaa nae kwenye daladala,
NikasimamaKumsikiliza
"Sorry mi naitwa Habiba, nakuona kabisa hauko sawa kakaang sijui naweza kukusaidia chochote "
"Ah acha tu Nashkur "
"Ooh sawa bas nyamaza usilie hvyo Jaman, mim nakaa huku chini sijui mwezangu unaitwa nan "
"Mi niite sancho, ila acha niwahi nyumbani,"
"OK Pole kwa kupitishwa mwaya ila kama hautojali chukua namba zangu endapo utahitaji msaada wangu utanitafuta"nikaitoa cm yangu , nikachukua namba yake nikaisevu bila kuandika jina kisha nikarudisha cm mfukon,
"Poa bye "
"Ok bye myn kua makini, "
Nikaenda upande wa pili wa dala dala nikakaa siti ya mwanzoni karibu na dereva,ili nisisumbuke kupisha pisha watu wakati wa kushuka, nilishtuka cm yangu ikiita nilipoitoa ni namba ya leyl@th ilikua ikiingia kwa hasira nikaiangalia kisha nikakata, hazikupita dakika nying akapiga tena napo nikakata na alipopiga mara ya nne nikazima kabisa cm yenyewe, nikawa nimekaa natafakar maneno yake makali yaliyonyima amani moyon mwang, gar ilitembea mpaka kituoni ninaposhuka nikaomba isimame kisha nikashuka, nikawa nasonga kuelekea nyumbani taratbu nikapita vichochoro vyangu nikajikuta nimefika, cha kushangaza na kilichonifanya nijikute nasimama kwa hasira ni baada ya kukuta gari ya leyl@th ikiwa imepaki nje ya kajumba chetu........ ItaEndelEaaaaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA WWW.DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments