Breaking News

REAL LOVE 💘.....SEHEMU 16


REAL LOVE 💘.....SEHEMU 16
ILIPOISHIA.....
Nikarudi nayo nyumbani na kumkuta suma zkijitahidi kumkokota mama ambaye alionekana kufumba macho na hajielewi, nilijikuta machozi yakinitoka nikiwa siamini ninachokiona 😰......
ENDELEA......
Nilishuka haraka haraka kumfata suma ambaye alimshika mama,.
"Vp suma mama..."nilijikuta napata kigugumizi,
"Amna tumuwahishe Mwanang wa moto sana "
Tukasaidiana kumpakiza kwenye ile bajaj kisha tukaondoka kwa kasi kumuwahisha mama ambaye bado alikua anahema na mapigo ya moyo yalikwenda taratibu sana, machozi nisiyoweza kuyazuia yalidondoka Kama Mtoto mdogo,
"Sancho Mwanang uclie Mbona anapona huyu, "
Alinitia Moyo Ismail, tulifika hospital tukapokelewa na maness wa dharura, wakamuweka kwenye kitanda maalum cha kutembea na kumuwahisha wodini, nilienda nao lakin kufika mlangoni tukasimamishwa kuashiria haturuhusiwi kuingia, sikua na hiana zaid ya kusubiri kwenye kabenchi maalum kalikowekwa kwaajili ya kusubiri wagonjwa japo hapakukalika lakin Ismail alinisihi nitulie, tulikaa kwa muda wa masaa mawili huku pirika pirika za madocta walioingia na kutoka ziliongezeka bila yoyote kutusemesha, alitoka doctor mmoja namkumbuka kwa Jina la Hancy aliyemtibu Leylath kipind namleta,
"Sancho vip Mbona upo hapa na leo, "
"Daaah doctor nimemleta mamaangu anaumwa sana 😪,"Niliongea hali ya kuwa machozi Bado yananitoka sana,
"Ngoja nikasimamie hlo ndugu atakua Sawa Ucjal Sawa "
"Sawa "aliniahidi doctor Hancy ambaye kidogo Alinitia moyo wa subira, nikawa nimekaa Kama yatima kichwani nina mawazo lukuki nisijue hata niwaze lipi kwan kifo cha Rahma nacho kilikuja kichwani japo mara chache chache, zilipopita dakika Kama kumi na tano alitoka doctor Hancy akionekana ana majasho meng sana,
"Vip doctor? "Tuliuliza mim na suma kwa shauku sana,
"Mama hali yake siyo nzuri kwakwel....."alisita kidogo "mwili wake umepararize upande mmoja, na anaonekana hana good balance diet, hivyo mwili wake umedhoofu na kusababisha saratani ya matiti, Yaan maziwa yake yanakansa kubwa sana, ambayo inatulazimu tumfanyie operation ya kuondoa nyama nyama ambazo zinachochea kansa hiyo kusambaa sehemu zengne za mwili,.... operation ya saratani ni sh.million 2 na nusu ndugu yangu na Bado dawa dawa za kuponeshea vidonda pia kulipia kitanda ili tuweze kuokoa uhai wake, "
Alimaliza doctor kwa kusema hivyo,
Mwili ukajihisi kupoteza nguvu, nikawa napata mawazo meng na nilishaanza kuhis namkosa mamaangu hivi hivi, kwan million hizo nitazitoa wapi Mlatino mie,
"Sasaa doctor,... "
"Yaan sancho mama anabidi afanyiwe operation kesho so Kama una uwezo wa kupata million hata moja njoo nayo kwakua mim Ndo now nimechukua majukum ya kumtreat mom ntalismamia, vinginevyo tukimchelewesha tutampoteza mama sancho, "maelezo ya doctor yakanichanganya kabisa nisijue cha kukifanya kwa usiku ule ili nijipatie hiyo million moja, akilini nikawaza nilichukuaga sh.laki tano na nusu kwa Rahma lakin tokana na mishe mishe za huku na kule bilibaki na laki tano Kama na elfu kumi tu,
"Doctor laki tano je?! "
"Sancho operation hua haihitaji kulipa kidogo kidogo coz washughulikiaj ni wengi na wanataka in cash nimesema million moja nikimaanisha wengine watalipwa mim nitasubiri na kuna wengine waelewa ndugu yangu jtahid, "
"Sawa doctor siwez kumuona hata kidogo "
"Tumempa dawa muache apumzike,
"Sawa doctor, nilijikuta naondoka Kama mtu aliyechanganyikiwa huku nikifatwa na Ismail ambaye muda wote wa maongezi yetu alikaa kimya,
"Oya sancho mbona speed Kama hivyo damu yangu "
"Daaah Mwanang nimechanganyikiwa "
"Acha kujichanganya simama tuwaze tunapata vipi hiyo hela usiku huu ndugu yangu syo useme umechanganyikiwa,"
"Mamaangu Suma,...😭"
"Sancho usilie sasa haya matatzo yapo na ww ni Mtoto wa kiume hebu jikaze bhana "
Alinibembeleza huku akinifuta machozi ,
"Haya tunafanya nn Mwanang sancho manaake hapa tukisema tungojee kesho hiyo hiyo syo rahisi, "
"Twende nyumbani kwanza, "
"Poa "
Tulikubaliana na kushika njia ya kurudi nyumbani, tulipita chochoro chochoro kwa mwendo wa haraka Kama maaskali waliotoroka depo, ndani ya nusu saa tukawa tumefika nyumbani, niliingia chumbani moja kwa moja, na kuchukua suruali ile niliyovalia nilipotoka Kwa Rahma, nikaisachi nikakuta shilingi laki tano na elfu ishirini japo namimi nilirudi na shilingi elfu tatu baada ya kulipia bajaj, nikashtukia kukuta kitu kigumu kwenye suruali yangu nilipotazama nikakumbuka ni kadi aliyonipa Pendo, nilipotazama kwa makini nikagundua kuna namba za cm, nikatoka haraka haraka nikiwa nawazo la kutafuta cm,
"Wapi sasa sancho? "
"Suma Wew kapumzike damu yangu Nashkur sana kwa msaada wako, acha mi niende sehemu flani hivi nikafatilie hela, "
"Sancho huna haja ya kunishukuru kwani mama yako ni mama yangu pia kumbuka alivyotulea Kama mapacha japo skua mwanae, shida ngapi kanisaidia mamaako, kanipa chakula nilipokua nanjaa mamaako leo nikuachie hili swala peke yako Kwel kaka siwez Mwanang nikawa mchoyo wa fadhila kias hicho 😪"aliongea Ismail kwa uchungu sana huku machozi yakianza kumtoka Kama Mtoto kias alinifanya nami nianze kulia nisijue cha kumwambia,
"Suma mchango wako ni zaid ya ndugu kwangu wew Ndo ndugu pekee wa mim, Usijal tupo Pamoja kuna mtu nataka numfate Kwahyo hatuwez kwenda wawili kaka Wew fanya mpango Kama vip na mim nifanye ili tujue kesho tunawasilisha nn kaka "niliongea kwa kujikaza na kumfanya Suma anielewe kisha tukaagana nikielekea nisipopajua ........ itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments