KAULI YA DIAMOND BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA
Diamond akiwasili mahakamani hapo.
“Hii haikuwa kesi, bali tuliitwa kusuruhishwa na mahakama, hivyo tumeenda tukapatana, hapa tumekuja tena leo kwa ajili ya kuweka sawa kumbukumbu za mahakama ili isije ikatokea leo na kesho kikazungumzwa kitu kingine ambacho kitaleta shida.
“Ninawashauri wasanii wenzangu na wazazi kwa ujumla, jambo kama hili likitokea wasiweke majungu yao pamoja kwani watakayekuwa wanamtesa ni mtoto, badala yake waangalie namna bora ya kumsaidia mtoto wao,” alisema Diamond.
Post By: Dabest4G


No comments