Hizi hapa njia za kuamsha na kudumisha uhusiano
mzuri kati yako na mpenzi wako hasa baada ya kuwa mmeshazoeana sana na
kuhisi kuchokana.
Dumisha faragha katika mahusiano yenu
Hakikisha kunakua na faragha katika mahusiano yako
na mpenzi wako. Vile vile itahakikisha kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa
na wakati wa kutosha kustarehe bila wasiwasi. Usiruhusu siri zako na
mwanamke zitoke nje kati yenu.
1. Tenga muda wa kustarehe pamoja
Ili kudumisha mahusiano na mwanamke lazima kuwepo na
mda wa kuwa pamoja na kufanya mambo yenu mnayoyataka kwa kuridhika bila
kupungukiwa na muda. Kwa mfano ni muhimu kupumzika mapema kitandani ili
kuhakikisha mnakuwa na wasaa wa kutosha wa kufanya mapenzi.
2. Ongeeni pamoja kwa uhuru kuhusu suala la tendo la ndoa
Ni muhimu kujadili na kukubaliana na mwanamke kuhusu
swala la kufanya mapenzi. Ni vyema muongee kuhusu suala la mapenzi na
jinsi ya kuwasha moto wa mapenzi baada ya kuchokana. Mwanamke anatakiwa
apewe uhuru wa kusema kile anachokihitaji.
3. Pangeni miadi ya usiku
Mwanamke huridhika zaidi katika mapenzi kwa
kuandaliwa ipasavyo hii ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufanya
mapenzi. Hivyo ni vyema kupanga miadi ya usiku ili mwanamke awe tayari
na ili kumridhisha mwanamke.
4. Badilisha mazingira
Njia nyingine ya kuamsha mapenzi ni kubadili
mazingira ya kufanyia mapenzi. Kwa mfano mnaweza kuacha kitanda chenu
cha nyumbani na kulala katika chumba cha hoteli iwapo uamuzi huo
utaboresha mapenzi kati yenu.
Post By: Cc. DabestTz
👉 Jinsi ya kuamsha mahaba na mapenzi katika mahusiano👇✔
Reviewed by DabestMusic Media
on
February 07, 2018
Rating: 5
No comments