Baada ya kufuta picha za Diamond Platnumz, Rick Ross atoa neno
Rapa maarufu duniani Rick Ross wiki hii amefuta karibia picha zote za
msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambazo awali alikuwa ameziposti
kwenye ukurasa wake wa Instagram kitu ambacho kilizua gumzo kwa
mashabiki wake nchini Tanzania.
Rick Ross na Diamond Platnumz
Kama ulikuwa unaamini kuna bifu kati ya wawili hao, ukweli ni kwamba
wawili hao bado wapo kwenye mahusiano mazuri ila ni ishu tu za
kibiashara ndio zimewatenganisha kwa sasa ndio maana alifuta picha hizo.
Kwani Rick Ross jana alitumia muda wake kutoa maoni kwenye posti ya
Tarehe 01 Desemba 2017 ambapo aliweka promo ya wimbo mpya wa Diamond
kipindi hicho akiwa amewashirikisha kundi la Morgan Heritage
‘Hallelujah’ na kuandika kuwa “Diamond iz a Legend“.
Hata hivyo, kuthibitisha hilo kuwa Rick Ross na Diamond wapo poa ila ni
ishu tu za kibiashara ndio zimepelekea Rick Ross kufuta picha hizo, Moja
ya mameneja wa Diamond, Sallam amethibitisha hilo kwa kuandika
“Nafahamu mastaa wengi wakiposti vitu vya support au tangazo ikifika
muda wanafuta hata Diamond mwenyewe anafuta zikishapita muda wake“


No comments