REAL LOVE 💘.......SEHEMU 26
REAL LOVE
ILIPOISHIA......
Alinikaripia kwa sauti iliyojaa besi la kiume nilipomtazama macho yake yalikua mekundu kama katoka aliyevuta ganja ya Arusha sura yake iliiva na kuwa nyekundu mapigo ya moyo nikiwaza cha kufanya nikagundua kuwa alikuwa siyo yeye Bali ni mashetani yalikwishampanda kwan alitoa mingurumo kama simba.......
ENDELEA..............
Nilijawa na uwoga nisijue cha kufanya huku leyl@th akizidi kuunguruma huku akianza kujigongesha ukutani mara kadhaa, ilinibidi nimuwahi mikono yake na kumshika kwa nguvu sana, nilishtukia teke moja la tumbo lilinifanya nickie maumivu makali sana lakin sikujali kwan leyl@th alizidi kujigongesha gongesha kama mtu aliyevurugwa nikamlukia tena na kumkamata kwa tabu huku kukulu kukulu zilikua nyingi zikiambatana na mabao mateke, ngumi zilizoniumiza sana, kwa nguvu zangu zote nilizoumbwa nazo nilijikuta namdhibiti leyl@th kwa kumkalia juu ya kiuno chake huku yeye akiwa amelala juu ya kiuno chake, nikalivuta shuka kwa taabu kisha nikamfunga mikono yake na miguu kama furushi la nguo kisha nikamuacha akukuluke, saut ya kunguruma ilianza kupotea na moyo wa huruma uliniingia tena kadri nilipomtazama leyl@th jins alivyoonyesha kuchoka na jinsi nilivyomfunga funga kama mzigo wa kuni,alinguruma tarar'tbu huku akinitolea jicho la upole sana, nikamsogelea,
"Mpenz unashida gan lakn "nilimsemesha kwa upole, hakika nilitaman kukimbia baada ya kuckia kicheko kikali kilichoumiza masikio yangu nikaanza kutetemeka kama nipo mlima Kilimanjaro uchi, jasho la matatizo lilinitoka kama nipo kwenye ovena, akili yang ikanituma nimtafute Nuuran kwenye cm ya leyl@th,nilichukua mkoba wake haraka haraka nikachukua cm yake na kuanza kujarbu kuibofya lakin nilishindwa kwan iliwekwa lock, niliwaza huku nikimtazama leyl@th aliyezidi kunibabaisha na sauti zake za ajabu ajabu, kabla cjafanya kitu nilisikia mlango ukigongwa kwa nguvu huku mtu akiongea,
"Dadaa Dadaa da Leyl@th "
Niliinuka haraka haraka kwenda kumfungulia kwan nilijua kabisa ni Nuuran,
Nilimfungulia moja kwa moja akapita bila kunisemesha mpaka alipo leyl@th,
"Daah dadaang jamn,nilisahau yan
"Kwan kuna nn Nuuran
"Daah mambo ya kifamilia haya Shemej tutaongea baadae wacha tumpe dawa kwanza
"Dawa gan sasa
"Lete begi lake "nikachukua haraka haraka nikamkabidhi, akafungua kisha akatoa kichupa kidogo,
"Mfungue hilo shuka, "nikafanya kama nilivyoagizwa kwa umakin sana, nikamshika mikono kwa nguvu zangu zote nikisaidiana na Nuuran aliyemshka kwa mkono mmoja huku akiwa ananusisha kile kikopo chenye harufu kali, nilistaajabu kusikia vilio vya aina tofaut toka kwa leyl@th aliyekuwa analalamika kwa tabu sana, hakika nilikumbuka kua nami nimeumbwa na mwenyeez mungu ndiye muweza nikajikuta nasali peke yang kimoyo moyo nikashangaa kusikia kelele zikizidi na vimbwenga vya leyl@th vilizidi kunitisha,Nuuran yeye aliendlea kumfanyia vile huku akiongea kiarabu arabu nisichokielewa hata kidogo, masaa yalizid kwenda na usiku ulihitimu saa sita na...
Hali ya leyl@th ilizid kubadilika kadr muda ulivyozid kwenda leyl@th aliishiwa nguvu kabisa na kunyamaza kama mtu aliyepoteza fahamu, moyo ulipooza sana yani kwa kile nilichokiona nilijutia kumjua leyl@th,
"Shemej muachie yupo tear hapo "
"Sawa, Sema kachoka sana anaonyesha eee "
"Lazima achoke kutokana na vitu vile, Sema Shemej hamjafanya chochote, "
"Ndiyo Shemej "
"Daah Shemej ujue mi nampenda sana da leyl@th halikadhalika dada anakupenda sana ujue, usimtese wala usijaribu kurudia kumsaliti tafadhali kwan mateso yake ndo kama hivi ulivyoona, ila Shemej sahv we jiandae uende home ,"
"Shemej kwan nikibaki kuna nn si tubaki tu wote "
"Shemej we nenda sababu ukibaki akiamka twaanza upya hapa "japo ckujua kwann aniambie vile haraka haraka nikavaa,
"Sasa Nuuran mi naenda "
"Poa Shemej nauli shika "alitoa wallet yake na kuhesabu noti kumi za elfu 10 kisha kunikabidhi,nikapokea nikataka kutoka,
"Shemej namba yangu "
"Alfu nilisahau Nuuran hiyo ni muhimu kwel "
Nilimpatia cm yangu akaiandika kisha akaisevu kabisa na kunirudshia cm, nikachukua nikakuta imeseviwa Shemej Nur "
Nikatoka huku nikihofia na kuwazia maneno ya Nuuran, nilipofka nje kuelekea kupanda gari, kabla cjafika kituoni nikasikia cm ikiita nilipoitoa namba ilikua ni ngeni,
"HALLO "
"HEE SANCHO JAMANI MBONA UNANIFANYIA HIVYO MY "
"NAN KWANZA MBONA CJAKUPATA UZUR "
"MI HONESTLY JAMANI "
"ANHAA NAMBIE "
"BADO HUJARUD TUU "
"DAAH NDO NARUD "
"NJOO BAS JMN MI NAKUNGOJEA "
"DUUH SAAHZI "
"YAA MI SIJALALA NAKUSUBIRI WEW, "
"TAFADHALI LEO SIPO SAWA TUFANYE KESHO "
"SANCHO MARA MOJA TUU KUNIONA MWENZIO MGUU UMEVIMBA "
"MMMMH BASI NAKUJA NGOJA NICHUKUE PIKIPIKI FASTA "
"POA USICHELEWE"nikakata cm kisha nikaanza kuelekea ilipo stend nikaiona bodaboda nikaismamisha na kupanda, haikuchukua muda mwing tukawa tupo nje ya nyumba ya Honestly tokana na mwendo kasi aliotumia, nililipa na kurudshiwa chenji nkaanza kumpgia cm Honestly ambye alikua hapokei cm, nikapiga mara kadhaa lakin ilikua vile vile, niliamua kuingia ndani baada ya kufungua mlango ule uliyoonekana kua wazi,nikahisi labda atakua amepitiwa na usingizi nikaingia mpaka chumbani lakini ckukuta mtu, nilishtuka baada ya kuxkia mlango ukifungwa nikatoka haraka haraka na kumkuta Honestly akiwa amevalia short sket ya kulalia yan kichupi chenye muonekano kilichofanya mapaja yake kua waz kwa kias kikubwa nikajkuta namtazama na kuduwaa....... ItaEndelEaaaaa
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA WWW.DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments