Breaking News

REAL LOVE 💘.....SEHEMU 19


REAL LOVE 💘.....SEHEMU 19
ILIPOISHIA.......
Alinijibu huku akizidi kulia huku akinikumbatia Mimi ambaye mawazo Yang yalihamia kwa mama yangu ambapo kichwani picha lake ilinijia taratibu.......
ENDELEA......
Moyo Wang akaanza kuishiwa nguvu,akilini niliwaza kua Pendo alikua ananiectia tuu, hata Kama sina uelewa wa mambo ya ATM lakin najua kua kuna namba za siri hua zinawekwaga,
"Wew ebu nickilize!, ucniletee ubongo muvi apa,Yan kunipeti peti kote kumbe ulikua na shida ya haja zako tuu alafu unajifanya hela zmeibiwa, umeniona mi zunde uongo, kwanza niachie 😠"
"Sancho 😨"
"Niachieeeee 😁"
Niliongea kwa gadhabu sana na kumfanya Pendo aogope,nikaondoka Kama shehe aliyelishwa nguruwe, moja kwa moja mpaka kwa Pendo nikachukua kilicho changu nikatoka speed japo nilimkuta nje akionekana kuniogopa,sikumsemesha nikapita Kama jini,
"Bby lakin 😪"
"Niache Pendo, ni bora ungeniambia Kama huwez kunisaidia kuliko kunifanyia hivi mim asubuhi hii naipata vipi laki tano Jaman 😭,usinijue tafadhali niache na matatizo yangu Pendo,
Niliondoka huku ninalia japo Pendo alionekana hakukusudia lile lililotokea, nikasonga kurud nyumbani kumfata suma tujue tufanyeje,nikapita kona zangu za hapa na kule nikakutana na zile njemba nilizowahi kuzidhulumu, lakin sikuogopa kwan nilishawalipa,
"Oyaa mlatino,Vip baba? "
"Shwari tuu, inakuaje wanangu "
"Daaah Fresh tuuu, ela yetu vipi? "
"Daaah hela gani wakubwa si tushamalizana "
"Usituzingue Mlatino tumemelizana lini "
"Alafu huyu dogo anajikuta mjanja mjanja sana, "
Waliongea huku wakinikwida hadharani ,
"Wanangu siku ile si niliwapa ela yenu lakin,"
Nilijitetea lakin walinikwida kwa nguvu huku mmoja akinisachi mfukoni,
"Weeeeziiii... iiii!!! 😫"
Niljaribu kupiga yowe japo hakuna aliyejotokeza nikashtukia nimepigwa ngumi moja ya mdomo na kufanya taya zilegee na kushindwa kupiga yowe tena, niliibiwa najiona yani nilishindwa hata kurusha ngumi Mtoto wa kiume nikajikuta nalia Kama Mtoto mdogo huku nikiwatazama washkaji ambao waliishia na fedha zote nilizokua nazo,
Akili ikaanza kuzunguka Kama feni, nikawaza meng juu ya mamaangu, nikawaza cha kufanya muda ule niliokua nimekaa chini nalia sana, mwili uliishiwa nguvu na nikajikuta napoteza fahamu, sikujua kilotokea nn lakin nilishtuka baada ya kumwagiwa maji nikakuta watu wengi wamenizunguka nikatazama kwa makini nikagundua ni sehemu niliyoporwa,
"Oyaa vip wewee "
"Kaka unajiskiajee "
"Uyoo ananjaaa huyo "
"Mwacheni bwana "
Walisikika watu tofauti tofauti walionizunguka mie ambaye nilikua nainuka Kama robot,
"Niacheni nipo Sawa tu!"
Nilisimama na kuanza kiondoka kuelekea nisipopajua kwan akili Bado ilikua inasachi, nilichanganyikiwa zaid baada ya kugundua kuwa ulikua mchana, nikaanza kutembea haraka haraka huku nikipata wazo la kwenda hospital kwanza, nilikimbia sana kwani sikuwa na pesa kwa muda huo niliongeza kasi ya kukimbia maana kutoka sinza had magomeni kuna umbali sana, nilijitesa kwa kukimbia kwenye jua lile kali, nikaanza kujikuta machozi yananitoka huku nikiwa nakimbia, kwan nilijiona nachelewa zaid,
Nilichukua takribani dakika hamsini mpaka kufika hospital, nikiwa nina majasho meng nikapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye wodi aliyokua amelazwa, nilishtuka baada ya kufungua mlango, sikukuta mtu nikatoka na wasiwasi mwingi nikielekea mapokezi nikakutana na ness mmoja aliyeonekana anaharaka sana,
"Samahani dadaang, "
"Eee ongea haraka kidogo nina mgonjwa ananisubiri "
"Mamaangu alilazwa wodi ile pale Mbona sijamkuta "
"Ameruhusiwa tayari, kaka acha niwahi "
"Karuhusiwa vipi wakati.... "
"Amechukuliwa "alidakia ness yule aliyekua akiondoka kwa madaha na haraka sana........ itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments