Breaking News

REAL LOVE 💘......SEHEMU 13


REAL LOVE 💘......SEHEMU 13
ILIPOISHIA.......
Nilishtuka nilipomkuta Rahma akiwa kadondoka chini na kitaulo chake huku damu ikiwa inamtoka maeneo ya kichwani.....
ENDELEA....
Nikamkilbilia pale alipokua ameanguka nikamkuta akiwa analia huku damu zkiwa znatoka sehemu ya kichwa ambapo palioneka kuchanika, nikamuinua haraka haraka,
"Vp tena Rahma? "Niliuliza kwa hofu kidogo huku nikiwa namfuta futa damu na zile nguo nilizokuja nazo,
"Nimeteleza nikajigonga yan miguu yote haina nguvu mpenz "
"Pole sasa twende hospital au? "
"Yaah chukua hiyo cm yangu Kuna namba imeseviwa boda, ipige mwambie aje😪, "aliongea huku akiwa Bado analia,
"Pole bas nyamaza tunaenda sasa hivi, "nilichukua cm yake na kumpigia dereva wa boda boda kisha nikamuita,... ndani ya dakika tano dereva alikuja tukasaudiana kumkokota Rahma hadi tukampakiza haraka haraka tunaelekea hospital ile ile ya magomeni ambayo ni karibu sana na nyumbani kwake,
Ilishahitimu saa sita usiku ambapo tulikuta madocta wachache wa shift ya usiku, nao walitupokea na kuanza kumpa matibabu Rahma ambaye alishkiria nguo ile nliyompa mim kupunguza speed ya damu inayotoka kwa kasi, madocta wakatuamuru tungojee nje Mim na dereva boda boda tukabaki kwenye benchi special la kusubiria mgonjwa,
"Babuu imekuaje Kwan?! "Aliuliza dereva wa boda boda,
"Kajigonga alipokua anatoka chooni, "
"Kajingonga vipi sasa "
"Yaan kateleza alipokua anatoka chooni ndo akaanguka akapasuka!"
"Duuh kaumia sana inaonekana eee "
"Siyo kiivyo Sema uoga tu,si unajua watoto wa kike, "
"Mbona damu inatoka nying? "
"Damu ile kawaida hata Wew ukijichana kidoleni inatoka nying kama unakula mboga saba, syo kama mie mboga zangu zikizidi nne tena hapo, mlenda, dagaa, kachumbari na limao au ndimu ilochanganywa na pilipili baas asa Unadhan damu itatoka vipi kama vile "
"Hahahah 😂😂,mboga nne za kibabe uongo "
"Hivyo yani, "
Tukapiga story kadhaa pale mpaka akatoka doctor, tukasmama kupokea taarifa,
"Vip doctor hali ya mgonjwa? "
"Mgonjwa hali yake si nzuri sana Kwan amepoteza damu kias flan hivyo tumemshona nyuzi tatu na tumemuwekea damu na dripu ya maji hivyo atalazwa hapa, itabidi mlipie kitanda mpaka kesho mimfate "
"Duuh kuja kulipia kesho hyo hyo je maana hapa tumekuja haraka haraka, "
"Amna tatizo "
"Sawa basi doctor kesho"
Tukatoka na dereva moja kwa moja tukapanda boda boda,
"Tunaelekea wapi,? "Aliuliza dereva
"Twende nyumbani KWA Rahma mara moja"
Pikipiki ikawashwa na kuanza safar ya kuelekea nyumbani kwa Rahma ambayo haikuchukua muda mrefu tukawa tumefika,
"Ningojee, "
Nilishuka haraka haraka nikaelekea ndani kwenye jumba lile nikaingia had chumbani kwa Rahma nikatafuta handbag yake nikaiona juu ya dressing table nikaichukua na kuisachi,nikakuta shiling laki tano na elfu hamsini, nikaechukua nikatoka na kuzma taa zote za jumba lile kubwa lilolotisha usiku ule,nikarudi kwenye boda boda, nikapanda,
"Twende zetu "
"Wapi? Kwenu au "
"Yaah "
"Poa "
Pikipiki ikawashwa na safar ya kurud nyumbani ikachukua nafas yake, pia haikuchukua muda sana kwan magar yalikua ni machache sana barabarani hivyo msongamano haukuwepo, Ukifika hadi nje ya kajumba chetu, tuliagana na dereva boda boda nikaingia chumbani kwa mama moja kwa moja nikamkuta kajilaza zake nami nikaenda Kama kawaida nikamshushia neti na kumfunika vizur na shuka kisha nikaenda zangu kulala, nilipojitupa kitandani, sikupata tabu ya kuutafuta usingiz kwan nilichoka sana na pilika pilika zile, za mechi kali na Rahma, yule Pendo na hangaika za hospital zminichosha sana, kufumbua macho nilipata lugundua kua asubuhi ilishaingia kwan jua lilichukua nafas yake kutawala anga,...
Taratibu nikajikongoja nikatoka kitandani nikapiga mswaki nikaoga nikaenda kumuoangalia mama ambaye bado alikua kalala nikamuamsha kisha nikamnawisha maji uso wake, nikabandika maji ya chai kwenye jiko la mchina linalotoa moshi baada ya kuchoka na kuchakaa sana nikaenda kwa mama Rody Kununua vitumbua kisha nikamletea akawa anakula mim nikaaga na kuelekea zangu hospital na nguo zangu zile zile za jana ambazo kidogo zilionekana zina unafuu na zina muonekano japo zmechanika baadhi ya maeneo, kuliko zengne ni za kuokotea makopo tuu, nikaanza safar ya kuelekea hospital ,nikiwa naelekea kituo cha basi alikuja dereva yule wa boda boda,
"Panda twende!! "Nikaifata pikipiki ilopaki pembezoni kidogo nikapanda tukaelekea hospital fasta tulifika, nikashuka peke yangu kuelekea wodini kwan dereva yule wa boda boda aliendlea na biashara yake, nikasonga moja kwa moja kuelekea kwenye wodi aliolazwa Rahma, kabla sijaingia nilishtukia nikishikwa bega na mdada ambaye akili yangu ilivuta picha ya haraka haraka nikajua kua nilishawahi kumuona lakin sikukumbuka nilimuona wapi,
"Mambo Kakaang "
"Safi tu cjui Wew "
"Mi sipo Sawa kwa ulichonifanyia! "
"Nilichokufanyia?!! "Akili ilizunguka Kama tairi inayoshuka kwenye mlima kitonga nikapata picha kua yule ni Pendo...... itaEndEndE@
USIKOSE REAL LOVE KUTOKA DABEST4G.BLOGSPOT.COM

No comments