Neymar azua gumzo mtandaoni baada ya kushangilia hivi (+Picha)
Neymar amekuwa akiangazwa zaidi toka alipojiunga na matajiri wa Ufaransa
klabu ya PSG kwa dau nono la paundi milioni 200 na kwa sasa amekuwa
gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuonyesha staili yake mpya
ushangiliaji.
Baada ya kushinda bao lake hilo kwanjia ya mkwaju wa penati akaweka
kiatu chake chenye chata la Nike katika paji la uso wake kitendo ambacho
kimetawala katika vichwa vya habari huku watu wengi wakitumiana picha
hiyo.
Katika mchezo huo Neymar, Kylian Mbappe na Angel Di Maria wote wametupia
mara mbili na kuifanya Paris Saint-Germain kutoka na ushindi wa mabao
6-1 dhidi ya Rennes katika michuano ya French Cup siku ya Jumapili.

No comments