Halotel yafikisha 10% ya wateja wote wa simu nchini
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano , Mhina Semwenda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
KAMPUNI ya Halotel Tanzania imetangaza
kuendelea kupata mafanikio na kuongezeka kwa kasi ya ukuaji katika
kipindi cha robo tatu ya mwisho ya mwaka 2017 na kufikia asilimia kumi
10 ya idadi ya wateja wote wa mitandao ya simu takwimu zinaonesha.
Katika Takwimu hizo za hivi karibuni,
zilizochapishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania
(TCRA), zinaonyesha kwamba namba ya wateja wa Halotel imekuwa na kufikia
milioni nne hadi Desemba 2017 katika soko la ushindani ambapo
makampuni saba ya simu za mikononi, yamekuwa yakishindana katika
kusajili wateja million 40 kwa kadi za simu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano , Mhina Semwenda amesema, haya ni mafanikio
makubwa kwa kampuni ya Halotel ambapo ndani ya miaka miwili wameweza
kufikia wateja wapatao Milioni tatu na laki nane hadi kufikia Septemba
2017.
Pamoja na wateja hao sehemu ya soko la
Halotel ilifikia kiwango cha tarakimu mbili ya asilimia 10 kutoka
asilimia tisa mwaka 2017. Hii ina maana kwamba kampuni hiyo iliyoanza
kutoa huduma miaka miwili iliyopita miaka miwili imeweza kupita baadhi
ya makampuni ambayo yamekuwa kwenye soko kwa zaidi ya miaka kumi.
Vile vile, kampuni imeweza kuongeza sehemu
ya soko katika huduma za kifedha kwa njia ya simu ( Halopesa) kwa
asilimia nne wakati wa robo ya mwisho ya mwaka 2017, ambayo imekua
kutoka kwa asilimia mbili tu kwa Septemba mwaka 2017 ilikuwa na jumla ya
milioni moja katika huduma yake ya halopesa hadi kufikia januari mwaka
huu.
Ukuaji huu mkubwa umekuwa ni mahsusi kwa
ukuaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu huku huduma ya HaloPesa
kuwa miongoni mwa huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni ya simu.
Uongozi wa kampuni hiyo ya simu umeeleza
kuwa mafanikio haya ni sehemu ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni
hiyo sambamba na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na mamlaka
husika.
“Tunajivunia kiwango cha ukuaji wa haraka
na mkubwa zaidi ambao tumepata kuushuhudia miongoni mwa makampuni ya
simu nchini na Afrika kwa ujumla. Tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika
kipindi cha miaka miwili na ukuaji huu ni ushahidi tosha wa uwekezaji
huu,” alisema Mhina.
Hivi karibuni waandaaji wa tuzo za
Kimataifa kwa kampuni mbalimbali duniani (Stevie Awards 2017) waliweza
kutambua kiwango cha ukuaji wa kampuni ya Halotel Tanzania na kuitunuku
tuzo ya kimataifa ya kibiashara iliyotambulika kama “Kampuni inayokua
kwa kasi zaidi kibiashara katika ukanda wa nchi zilizo Mashariki ya Kati
na Afrika kwa mwaka 2017.
Kampuni hiyo, kwa mujibu wa Semwenda
imewekeza dola milioni 800 (takribani Sh1.7 trilioni) katika upanuzi wa
mtandao na kuboresha huduma za mawasiliano nchini Tanzania tangu Oktoba
2015, huku wakiweka malengo ya kuanzisha huduma za 4 G LTE pamoja na
huduma nyingine za Mawasiliano.
By: Dabest4G

No comments