BAADA YA TUNDU LISSU KUMWAMBIA LEMUTUZ ASILAZIMISHE URAFIKI NAYE,LEMUTUZ AMJIBU HIVI TUNDU LISSU
ALICHO ANDIKA TUNDU LISSU
- tundulissutz LEMUTUZ ASILAZIMISHE URAFIKI USIOKUWEPO!!! .
Leo nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz.
Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa.
Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. .
Amewaambia wasomaji wake kwamba alinichukua kwenye gari yake binafsi kutoka JFK hadi Connecticut kwenye graduation ya dada yangu aliyodai ilikuwa Connecticut State University. .
Ili kuthibitisha kauli zake, Lemutuz ameambatanisha picha niliyopiga naye, ambayo nitaielezea shortly. .
Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa.
Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakumbuka vizuri, Lemutuz alikuwa MC kwenye shughuli hiyo. Na siku hiyo kulikuwa na Watanzania wengine wengi waishio Marekani. .
Lemutuz hakunipokea mimi JFK wala kunipeleka Bridgeport, Connecticut, kwenye gari yake binafsi. Hatukuwa tunafahamiana kabla ya kukutana kwenye graduation ya kaka Vince, siku kadhaa baada ya mimi, mke wangu na ndugu zangu wengine kuwasili Marekani. .
Pili, ni kweli tulipiga picha ambayo ameitoa kama uthibitisho wa ‘urafiki’ wetu. Siku hiyo, kama ilivyo kwenye shughuli kama hizo, nilipiga picha na Watanzania karibu wote waliohudhuria graduation hiyo.…. naendelea…………..
ALICHO ANDIKA LEMUTUZ
- lemutuz_superbrand LE MUTUZ MOBIMBA! …..LE MUTUZ CINTWAYEEN! …..LE MUTUZ BOMAYEEE….HAHAHAHAAHAHA…..KWANZA MWAKA 2011 NILIKUA NIMESHARUDI TANZANIA SIKUWEPO USA ….PILI CONNECTICUT MJINI TULIPOENDA KUNA CHUO KIMOJA TU CONN. STATE…and then Bridgeport College nje ya Downtown……TATU NISINGEWEZA KUTOKA NEW YORK MPAKA CONNECTICUT PEKE YANGU BILA SABABU SAFARI YA MASAA 3 NO WAY! …….HAHAHA NAONA NI JUST ….politics ….hahahaha ndugu yangu kwanza pole sana kwa masahibu yaliyokukuta …NIMEKUSIKIA LOUD AND CLEAR..Kaka yako alitokea Tanzania then akaja kukupokea JFK na kukupeleka Connecticut? ….hahahaha this is the biggest joke of my life …..NILIKUFANYIA WEMA AMBAO SIUJUTII PAMOJA NA KELELE ZAKO ZA MLANGO! … na pia ungesema yote ya jinsi nilipoenda Kijijini kwa Wazazi wako Mahambe/Singida nilikua nafuata nini wakati mimi na wewe hatuna mahusiano yoyote? AGAIN NILIKUFANYIA WEMA KAMA RAFIKI NA SIUJUTII KWA SABABU YA KELELE ZAKO ZA MLANGO … ..hahaha…halafu pia ungesema tulipoanzia kukutana kwenye Vita ya Jamiiforums ulipokuwa Mwanasheria wetu si ndiko tulikoanzia mbona hukusema hiyo tulipokua tunapigana kuwatoa ndani jamaa zetu au umesahau kwa sababu ya Politics? ..mara ngapi ulinibembeleza nimuombe Waziri Lau Masha awaachie? Umeshasahau? …hahahahaha…..ni kweli mara ya mwisho tulikutana Ofisini kwa Bosi wako Mbowe ukalalamika sana kwamba mimi ni “CCM MAGAMBA” na hutaki Urafiki tena sawa ila haifuti record ya tulikotokea …MUOGOPE MUNGU KIDOGO hahahaa lakini NIMEKUSOMA ..NAKUOMBEA MUNGU AKUTANGULIE UPONE HARAKA! …hayo mengine ni Politics as Usual nimekuelewa!…..ILA SISHANGAI KUMBUKA MANENO ULIYOYASEMA ALIPOKUJA KIONGOZI MMOJA WA TAIFA WA CCM PALE KITANDANI KWAKO HOSPITALI YA NAIROBI ….SI ULIWAKANA CHADEMA UKASEMA NI MANENO YAO TU MITANDAONI WEWE HUNA TATIZO NA SERIKALI YA CCM AU UMESAHAU? kumbe kukana watu ni tabia yako kwa sababu ya politics? ….DUH!..HAHAHAHA….pole sana ndugu yangu nakuombea Upone haraka!….NA THIS CASE IS CLOSED ON MY PART it is CHILDISH!..na unahitaji matibabu zaidi maana Graduation ya Dada unasema ilikua ya Kaka? lahaula .HAHAHAHAHA! …again THIS CASE IS CLOSED ON MY PART! – le Mutuz

No comments